Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Ahmed Abbas Ahmed, kusimamia utekelezaji wa Mkataba wa Usambazaji wa umeme katika Wilaya ya Newala, unaotekelezwa na Kampuni ya Central Electric International.

Waziri Mkuu ameyasema hayo wakati akiongea na wananchi wa Halmashauri ya Mji wa Newala, akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Mtwara huku Meneja wa TANESCO mkoa wa Mtwara Mhandisi, Tawakal Rwahila akisema Mkandarasi huyo alipaswa kukamilisha kazi hiyo Apriri 2023.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Mhandisi Rwahila amesema, mkandarasi huyo alipewa kazi ya kusambaza umeme katika vijiji 70 vya wilaya ya Newala Agosti 2021 na amekuwa na utendaji usioridhisha.

Aidha, Waziri Mkuu pia amekukagua maendeleo ya ujenzi wa majengo ya uboreshaji wa utoaji wa huduma za afya katika hospitali ya Mji Newala uliogharimu shilingi milioni 800.

Wakulima msiuze Korosho ghafi - Waziri Mkuu
Wingu zito lazidi kugubika mzozo wa Niger