Wakulima zao la Korosho wametakiwa kufanya kilimo cha kibiashara kwa kuacha kuuza Korosho ghafi na badala yake wauze zilizobanguliwa, ili kujiongeza tija zaidi.

Wito huo, umetolewa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati akiongea na wananchi wa halmashauri ya Mji wa Newala akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Mtwara, toa wito kwa wamiliki wa viwanda vya kubangua korosho watoe nafasi kwa wakulima kwenda kubangua korosho zao na kuwatoza gharama za ubanguaji.

Amesema, “wakati umefika tutumie fursa hii kujenga viwanda vya kubangulia korosho na Wakulima wabangua na kuuza katika masoko ya nje na ndani, bei ya kilo moja ya korosho iliyobanguliwa ni Shilingi 13,000 na ghafi ni Shilingi 2,000, ukibangua kilo nne za korosho ghafi unapata kilo moja ya ya korosho iliyobanguliwa.”

Amesema kitendo cha kusafirisha korosho ghafi nje ya nchi kinawakosesha baadhi ya mapato yatokanayo na maganda ya Korosho, ambayo yanatumika kutengeneza mafuta.

Julio aitahadharisha Simba SC
Majaliwa aingilia kati usuaji mradi wa kusambaza Umeme