Kamati ya Usalama Wilaya ya Mlele Mkoani Katavi imewakamata watu 67 wakiwemo raia 65 wa Ethiopia, ambao wameingia nchini bila kibali, dereva mmoja na dalali mmoja ambao walikua wakiwasafirisha kwenda Tunduma kwa kutumia Lori la Mafuta.

Akizungumza mara baada ya kukamatwa watu hao, Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama Wilaya ya Mlele ambaye ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Alhaj Majid Mwanga amesema watu hao wamekamatwa katika kizuizi cha Kamsisi kata ya kamsisi Wilayani Mlele Mkoani Katavi, barabara ya Tabora – Mpanda.

Amesema, kukamatwa kwa watuhumiwa hao kunatokana na ushirikiano mzuri kati ya Serikali na Wananchi kwani walipata taarifa kutoka kwa raia wema kuwa kuna lori la Mafuta lenye namba za Usajili T 952 DFD ambalo linatokea Mwanza Kuelekea Tunduma limebeba wahamiaji hao ndani ya Tanki.

Kwa upande wake dereva wa gari hiyo, Sadick Msomolo amesema hii ni mara ya kwanza kufanya kazi hiyo na alipewa mbinu hizo na kaka yake ambaye alikua dereva wa malori ambapo Kamati ya Usalama imewakabidhi watuhumiwa hao kwa Jeshi la Uhamiaji, kwa ajili ya Taratibu zingine za kisheria.

Cadena afichua siri nzito kwa Ally Salim
Hasheem Ibwe: Endeleeni kuibeza Azam FC