Kocha Mkuu wa Azam FC Youssouf Dabo ameondolewa kwenye orodha ya Makocha watakaokaa kwenye Mabenchi ya Ufundi wakati wa Michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara 2023/24, ambayo rasmi imeenza leo Agosti 15.

Dabo ambaye alianza kazi rasmi Azam FC wakati wa maandalizi ya msimu mpya ‘Pre Season’ ameenguliwa kwenye orodha hiyo, kufuatia kukosa vigezo vya taaluma vinavyotambuliwa na Shirikisho la Soka Tanzania ‘TFF’ na lile la Barani Afrika ‘CAF’.

Kocha mwingine aliyeenguliwa kwenye orodha hiyo ni Kocha Msaidizi wa Simba SC Ouannane Sallami pamoja na Kocha wa Viungo Corneille Hategekimana. Naye Kocha Msaidizi wa Young Africans Moussa Ndaw amepitiwa na panga hilo, sambamba na Kocha Mkuu wa Coastal Union Mwinyi Zahera.

Ally Kamwe: Yajayo Young Africans yanafurahisha
Mtibwa Sugar waitambia Simba SC Morogoro