Mabingwa wa Soka nchini Ujerumani FC Bayern Munich wanaweka mipango yao sawa kwa ajili ya kumnasa Mlinda Lango wa zamani wa Manchester United, David de Gea.

Mhispaniola huyo amekuwa huru tangu mkataba wake ulipofika kikomo huko Old Trafford mwishoni mwa mwezi Juni.

De Gea mwenye umri wa miaka 32, amekuwa akiripotiwa kuwa kwenye rada za klabu za Saudi Arabia, lakini sasa huenda akatua Allianz Arena.

Ripoti zinadai mabingwa hao wa Ujerumani wapo kwenye mazungumzo na De Gea kwa ajili ya kujiunga kwenye timu yao.

Hata hivyo, imeripotiwa kuwa na kikwazo kinachotishia kushindwa kukamilika kwa dili hilo kwani De Gea anahitaji kulipwa mshahara mkubwa kitu ambacho FC Bayern Munich hawatakuwa tayari.

Mlinda Lango huyo alikuwa mchezaji anayelipwa pesa nyingi zaidi kwenye kikosi cha Man United, alikuwa akipokea Pauni 375,000 kwa juma.

Timber aongeza mashaka The Gunners
MAISHA: Bwawa la kuogelea Pombe kuponya jeraha