Beki kutoka nchini England Harry Maguire ameuvimbia Uongozi wa  Manchester United akitaka alipwe Pauni 15 Milioni kwanza, kabla ya kukubali kwenda kujiunga na West Ham United kwenye dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi.

Mabosi wa klabu hiyo ya Old Trafford walidhani kwamba wameshamaliza kila kitu kuhusu beki huyo wa kati baada ya kukubali ofa ya Pauni 30 milioni kutoka kwa Wagonga Nyundo hao wa London.

Uongozi wa Man Utd ulikuwa tayari kumlipa Maguire Pauni 6 Milioni ili aondoke klabuni hapo, lakini imekuwa tofauti na ilivyofikiriwa.

Taarifa kutoka Old Trafford zinaeleza kuwa Beki huyo amegoma na kutaka alipwe Pauni 15 Milioni kwa sababu huko anakokwenda kwenye kikosi cha West Ham United atalazimika kupunguza mshahara wake kwa kiwango kikubwa.

Maguire atakapojiunga na West Ham United atalazimika kushusha mshahara wake kutoka Pauni 190,000 kwa juma hadi Pauni 120,000 kwa juma, hiyo itamfanya awe amelipwa pungufu ya Pauni 14.5 milioni kwenye dili lake la miaka minne.

Mkataba wa sasa wa Beki huyo kwenye kikosi cha Man United umebakiza miaka miwili ambapo angevuna kiasi cha Pauni 19.7 milioni.

Na sasa beki huyo wa kimataifa wa England mwenye umri wa miaka 30 haamini kama ofa aliyopewa ya kulipwa na Man United, Pauni 6 Milioni ili aondoke kuwa inatosha.

Tabora United yapigwa nyundo kusajili
Timber aongeza mashaka The Gunners