Baraza la Michezo Tanzania ‘BMT’, limetoa wito kwa vyama vya michezo nchini kujiimarisha katika eneo la utawala bora, mipango na kusimamia mwenendo wa chama.

Akizungumza jijini Dar es salaam, Katibu Mtendeji wa baraza hilo, Neema Msita, amesema vyama vya michezo vinapaswa kuandaa na kuweka mikakati ya kuendesha vyama hivyo kabla ya kuomba mahitaji mbalimbali kwani uendeshaji wa shughuli za michezo una gaharama kubwa, serikali haiwezi kubeba mzigo wa vyama vyote.

Neema amesema ni wajibu wa kila chama kuwa na mipango, taratibu za kujiendesha bila kutegemea serikali kwa asilimia 100.

Karim Mandonga yupo huru, kuzichapa Znz

Amemsema endapo chama kitajitengenezea mazingira mazuri ya kujiendesha, itakua rahisi kuwavutia wawekezaji na wadau kutoa sapoti. “Hakuna mwekezaji atakayekwenda kuwekeza katika chama kisichokuwa na mipango na mikakati, huu ni muda wa viongozi kuchangamka na kuacha kuitegemea serikali katika kila kitu,” amesisitiza Neema.

Singida Fountain Gate imedhamiria Afrika
Rejesheni fedha za kigeni kuimarisha uchumi - Biteko