Makumi ya Walimu, Wanafunzi na Viongozi wa Muungano wa Wafanyakazi mjini Miami jimbo la Florida nchini Marekani, wameandamana hadi makao makuu ya elimu wakilalamikia mfumo mpya wa somo la Historia ya watu weusi.

Waandamanaji hao, wanapinga mtaala huo ambao unahitaji Walimu kuwafundisha Watoto wa Shule za Msingi kwamba watumwa walijifunza maarifa ambayo yanaweza kutumika kuwasaidia katika maisha yao ya kila siku.

Gavana wa Florida Ron DeSantis ambaye ananuia kugombea urais mwaka ujao kupitia chama cha Republican, amekuwa akitetea mtaala huo akisema wakosoaji wake wakiwemo Naibu Rais, Kamala Harris na Wabunge wawili weusi wanapotosha watu, kwa kuutafsiri mstari mmoja wa mtaala huo.

Mmoja wa Viongozi wa maandamano hayo ambaye Profesa wa Saikolojia wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Florida, Marvin Dunn amesema hawatakubali watoto wao wafundishwe kuwa utumwa ulikuwa na manufaa kama ilivyopendekezwa na Gavana DeSantis.

Serikali yavipiga marufuku vyama vyote vya Siasa
Makabi Lilepo anavyowindwa Young Africans