Wizara ya afya nchini Sudan Kusini, imesema Watoto zaidi ya 70 wamepoteza maisha kwa kipindi cha wiki tatu zilizopita kutokana na kuugua ugonjwa wa Surua ambapo tangu kuanza kwa mwaka huu, ugonjwa huo umekuwa ukiripotiwa katika majimbo mbalimbali.

Daktari, Abdallah Faheem kutoka jimboni Jonglei amesema ugonjwa huo umeliathiri zaidi jimbo la Unity na kwamba wamegawana majukumu ili kuokoa waathiriwa na Daktari mwingine aitwaye Duol Biem, tayari anasimamia shughuli za afya katika eneo hilo.

Amesema, ‘‘ugonjwa wa surua umezuka katika kaunti kadhaa na majimbo. Surua ilipozuka, magonjwa mengine kama kuharisha yanaweza kutokea. Motto anaweza kupata ugonjwa wa nimonia. Surua inaambukizwa na kuenezwa haraka kutoka binadamu hadi binadamu mwingine.”

Hata hivyo, ameongeza kuwa, “kampeni kubwa inaendeshwa na wafanyakazi wa wizara ya afya. Tunachohitaji sasa ni washirika wa kimataifa kutusaidia wakati huu wa kampeni. Kila mtoto anahitaji chanjo. Nawasihi wazazi wajitokeze kwa wingi na watoto wao wachanjwe.’’

Hata hivyo, Watalaam hao wa afya wanaonya kuwa iwapo watoto walio chini ya umri wa miaka mitano, hawatopata lishe nzuri, itakayowasaidia kujikinga na ugonjwa huo, hali itaendelea kuwa mbaya.

Wachezaji Young Africans wanaitaka CAF
David Raya afichua siri nzito Arsenal