Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amevunja uongozi wa Soko la Mabibo na kuagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa – TAKUKURU, kufanya uchunguzi ili kuwabaini wabadhirifu na hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya wahusika.

Chalamila ametoa kauli hiyo mara baada ya kufika sokoni hapo kwa ajili ya kusikiliza na kutatua mgogoro baina ya wafanyabishara wasiowaaminifu wanaokingiwa kifua na Uongozi wa Soko hilo na Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.

Akiwa Sokoni hapo, Chalamila pia amekemea watu wanaokwamisha jitihada za Serikali kutojaribu kufanya hivyo kwani ni lazima soko hilo liboreshwe na mapato yakusanywe huku akisema hakuna mfanyabiashara atakayeondolewa wala kupandishiwa tozo ya ushuru.

Hata hivyo, Mkuu huyo wa Mkoa amebainisha kuwa Rais Dkt. Samia ana dhamira ya kuboresha masoko hivyo asitokee mtu mmoja kwa maslahi yake binafsi kutaka kukwamisha zoezi hilo na kwamba hawatasita kumchukulia hatua za kisheria.

Neymar afichua sababu ya kutimkia umangani
Kasongo: Hatuhusuki, ni uzembe wa Kitayosce