Abel Paul, Jeshi la Polisi – Dar es Salaam.

Jeshi la Polisi kikosi cha Afya limesema limekuwa likitoa huduma za kiafya kwa wananchi, Askari na familia zao wa maeneo tofauti licha ya kuwa na kazi yake ya msingi ya kuwalinda raia na mali zao na kupongeza hatua ya Askari kwa kuwafariji Wagonjwa wa Hosptali Kuu ya Jeshi la Polisi, iliyopo barabara ya kilwa jijini Dar es Salaam.

Hayo yamebainishwa na Afisa Mnadhimu namba moja wa kikosi cha Afya Kamishna Msadizi wa Polisi na Daktari Bingwa wa magonjwa ya kike,
ACP Salum Luyeko na kuongeza kuwa Askari hao wameonesha moyo wa pekee na kuwaomba kuendelea kutoa misaada zaidi kwa jamii.

Amesema, makundi mengine pia yanatakiwa kufika katika Hospitali hiyo ambayo inatoa huduma kwa makundi yote bila kubagua, huku akiongeza kuwa Askari hao pia wameonesha njia kwa wengine wanaopaswa kutembelea Hospitali kuu ya Jeshi la Polisi.

Kwa upande wake Mkufunzi toka Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam – DPA,
Mkaguzi Msaidizi wa Polisi A/Insp Isack Mulilo  amesema  wameona vyema kuungana kwa pamoja kutoa mchango wao na kufariji wagonjwa Hospitali kuu ya Jeshi la Polisi.

Naye Mwanafunzi wa kozi ya Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Aisha Wisley amesema wamekuwa na utaratibu huo kila mara kutoa msaada kwa makundi tofauti ndani ya Jamii na kwa kipindi hiki waliona watoe msaada na kuwafariji wagonjwa hao.

Mfuko uwekezaji wa Umma kupunguza utegemezi kwa Serikali
STAMICO yabeba tuzo mbili utendaji wenye tija