Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania – JWTZ, limesema taarifa iliyosambazwa katika mitandao ya kijamii kwamba wanajeshi wa ngazi za juu wa JWTZ wameongezewa mshahara ni taarifa ya uzushi na upotoshaji.

Taarifa ya Kaimu Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano Makao Makuu JWTZ, Luteni Kanali Gaudentius Gervas Ilonda imeeleza kuwa taarifa hiyo iliyosambaa ni uzushi na uchunguzi kwa waliosambaza unaendelea.

“Taarifa hiyo imeeleza kuwa limelipwa tarehe 18 Agosti 2023, JWTZ inaujulisha Umma kuwa taarifa hiyo ni ya uzushi na upotoshaji wa Jamii hivyo Watanzania waipuuze kwani ina nia ovu”

“Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania linaendelea na kuweka kwa kina aliyehusika na upotoshaji ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yake”

Tusiingize udini kwenye Siasa, tutafakari - Rugambwa
Wafariki kwa kutumbukia shimoni wakiwa harusini