Wachimbaji na Wafanyabiashara wa Madini wa Tanzania, wameendelea na ziara yao Nchini China ya kujipatia ujuzi na kutafuta Wawekezaji huku wakitembelea Makampuni yanayozalisha Vifaa vya Kuchimba na kuchenjua Madini, kushiriki vikao mbalimbali vya Viongozi, Makampuni na Viwanda, na kuingia makubaliano ya Kibiashara yanayolenga kukuza Sekta ya Madini Nchini.

Naibu Katibu Mkuu Mbibo, amesema Tanzania na China wana urafiki wa muda mrefu unaounganishwa na Viongozi wa Nchi zote mbili, akiwemo Rais China Xi Jinping na Rais Tanzania, Dkt. Samia Samia Suluhu Hassan, hivyo ni muhimu kuimarisha ushirikiano huo kwa vitendo ikiwemo kubadilishana uzoefu wa Teknolojia, kuboresha, kuongeza thamani na kuiinua sekta ya Madini.

Kadhalika Mbibo amewaalika Mameya, Wawekezaji na Wadau wa Madini kwenye Jukwaa Maalum la Wadau wa Madini linalotaraji kuanza mnamo mwezi Oktoba Mwaka huu, ikiwemo kutoa Mualiko Maalum wa Kiserikali, huku Meya wa Jimbo la Shandong, Zhang Dong akiishukuru Serikali ya Tanzania na kuahidi Ushirikiano pamoja na kufanya maandalizi ya kushiriki kongamo maalum la mwezi Oktoba nchini Tanzania.

Kwa upande wake Rais wa Jumuiya ya Wachimbaji Wadogo wa Madini Tanzania – FEMATA, yenye wananchama zaidi ya milioni 6, ameeleza kuwa Tanzania ina zaidi ya aina za madini 200, hivyo anawaalika wawekezaji kuja kuwekeza na kushirikiana na Wachimbaji Wadogo.

Uwekezaji huo, ili kuwaongezea ujuzi wa Teknolojia kwenye Sekta ya Madini huku akieleza kuwa juhudi za Serikali na Ubalozi wa Tanzania Nchini China umefungua milango yenye tija na anaamini kuwa sekta ya Madini itachangia zaidi pato la Taifa kwa hatua hizi zinazoendelea kuchukuliwa.

Ziara hiyo ya siku kumi, inajumuisha Wachimbaji takribani mia moja na Viongozi wa Serikali na Sekta Binafsi akiwemo Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Madini, Msafiri Mbibo, Konseli Mkuu wa Ubalozi wa Tanzania, Guangzhou pamoja na Rais wa FEMATA John Bina.

Wasiojulikana washambulia Kijiji, vifo watu 23
Tuhifadhi Mazingira maeneo ya Miradi - Dkt. Mkama