Kocha Pep Guardiola amesema alimwomnba shabiki wa Manchester City kuchukua nafasi yake kwenye benchi wakati wa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Newcastle United baada ya kukosolewa kwa kutofanya mabadiliko yoyote.

Guardiola alitoa ishara kwa shabiki karibu na benchi la City kuchukua nafasi yake kama kocha baada ya majibizano ya maneno.

Alifichua baadaye kuwa ni kwa sababu ya uamuzi wake wa kutofanya mabadiliko yoyote, ikiwa ni mara ya kwanza ameshindwa kufanya mabadiliko katika mchezo wa Ligi Kuu tangu Mei 2022.

“Alinitaka nifanye mabadiliko, mchezaji mmoja atoke na mwingine aingie, nikamuuliza yupi, sikujua,” alisema Guardiola.

“Nilisema njoo hapa uifanye. Niliona kwamba timu wakati huo ilikuwa bado hai na wakati mwingine kuingia.

“Niliona timu bado ipo na inapigania kila mpira. Wasimamizi, tunayo chaguo kufanya mabadiliko, lakini wasimamizi wanaamua au la.”

Guardiola alisema kabla ya mchezo dhidi ya Newcastle alikuwa na wasiwasi baada ya kuwapoteza wachezaji kadhaa muhimu akiwamo Kevin De Bruyne kutokana na majeraha.

Hata hivyo, Julian Álvarez alifunga katika kipindi cha kwanza na kupata ushindi wa bao 1-0 na kuhakikisha Man City inadumisha mwanzo wao, mzuri wa msimu kwa kushinda kwa mara ya pili mfululizo.

“Huu ni mchezo wa pili wa msimu huu, lakini ni uthibitisho wa sababu iliyotufanya tushinde sana,” alisema Guardiola.

“Mawazo ya kundi hili la wachezaji hunishangaza kila wakati. Dhidi ya timu hiyo na hali tunayofikia, tukiwa na majeraha mengi na hakuna kupumzika, walicheza vizuri sana. Jinsi wanavyolinda na jinsi wanavyokimbia na kujitolea kwa kila mtu ilikuwa ya kushangaza kabisa.”

Tabora Utd kamili kuivaa Singida FG
KMKM yataja sababu za kupoteza Kimataifa