Scolastica Msewa – Kibaha.

Mjumbe wa Halmashauri Mkuu ya Chama cha Mapinduzi – CCM Taifa M-NEC, Hamoud Jumaa amewataka viongozi na wana CCM kuhakikisha wanaongeza wanachama wapya kwa ajili ya kuimarisha uhai wa Chama na kujenga dhana ya kushika dola na si kupata ushindi.

Hamoud ameyasema hayo mjini Kibaha Mkoani Pwani, wakati akihutubia kwenye mkutano wa hadhara wa majumuisho ya ziara ya Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kibaha Mwajuma Nyamka ambapo alikuwa Mgeni rasmi.

Amesema, “nataka niwaambie ndugu zangu Chama lazima kihimalike na tuna misingi yetu ya Chama katika katika yetu kwenye ibala ya tano inazungumzia namna ya kushika dola na vyama vyote duniani nguzo yake ya msingi ni kukamata dola lazima tuongeze wanachama.”

Aidha, Hamoud ameongeza kuwa wanaCCM wanatakiwa kuhakikisha wanaongeza wanachama walio hai kwa kulipa ada za kila mwezi na kuwalinda wanachama wwaliopo, huku akidai kuwa wakati wa kushikamana umekaribia na wajiandae kushinda kwa kishindo chaguzi zijazo hasa zikiwemo za Serikali za mitaa mwakani.

Hata hivyo, Mjumbe huyo wa M-NEC amempongeza mbunge wa Jimbo la Kibaha Mjini, Silvestry Koka kwa kufanyakazi vizuri huku akimtaka aendelee kuchapakazi kwa ajili ya kutekeleza ilani ya uchaguzi kwakuwa CCM imeingia mkataba na wananchi na lazima isimamiwe vizuri.

Naye Mwenyekiti wa CCM Kibaha Mjini, Mwajuma Nyamka amesema chama hicho hakiwezi kujengwa na mtu mmoja hivyo wadau wanaojitokeza kuchangia wazingatie kufuata taratibu na kanuni na kwamba miradi ya maendeleo imetekelezeka kwa asilimia 90 na vikwazo kwa wananchi vimepungua.

Kwa upande wake Katibu wa Siasa na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Pwani, David Mramba amesisitiza umoja kwa wanachama ili kukiwezesha chama hicho kushinda kwenye chaguzi zijazo huku Mbunge wa Jimbo la Kibaha Mjini, Silvestry Koka akiwashukuru Wanachama, Mabalozi wa Mashina na Wenyeviti kwa kuendelea kushirikiana ili kukiimarisha Chama.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Agosti 22, 2023
Zimbabwe wafanya ibada kuombea uchaguzi Mkuu