Klabu ya Liverpool inaamin itafanikiwa kuipata saini ya kiungo wa Mabingwa wa Soka Ujerumani FC Bayern Munich, Ryan Gravenberch huku mazungumzo yakiendelea kati ya mabosi wa pande hizo mbili.

Kiungo huyo wa kimataifa wa Uholanzi anawindwa vikali na kocha Jurgen Klopp na anataka kukamilisha uhamisho huo haraka iwezekanavyo, kufuatia taarifa kueleza kuwa Manchester United inajitafuta kuiwinda saini yake.

Vilevile mazungumzo kwa ajili ya kiungo wa Crystal Palace, Cheick Doucoure yanaendelea kwa mujibu wa ripoti huku Gravenberch akifungua mlango wa kutoka Bayern.

Kiungo huyo Mholanzi mwenye umri wa miaka 21 alisajiliwa na Bayern kwa Pauni 21 milioni akitokea Ajax msimu uliopita, lakini alicheza mechi 33 katika mashindano yote tangu alipotua.

Man Utd yajitutumua Ulaya
Saba kizimbani tuhuma za wizi Bil. 1.23 Katavi