Manchester United imepanga kumsajili kiungo wa Mabingwa wa Soka nchini Ufaransa Paris St-Germain, Marco Verratti, katika dirisha hili la usajili lakini inakumbana na upinzani kutoka kwa Al-Ahli na FC Bayern Munich ambazo ndio zilikuwa za kwanza kuhusishwa na mchezaji huyo.

Mabosi wa Al-Hilal ya Saudi Arabia wanadaiwa walishatua Ufaransa kwa ajili ya mazungumzo ya kumsajili kiungo huyu lakini hawakufikia muafaka.

Man United imeonyesha nia ya kutaka kumsajili fundi huyu kwa sababu Fred ameondoka, huku kukiwa hakuna uhakika wa kuendelea kusalia na Scott McTominay, hivyo eneo lao la kiungo lina upungufu mkubwa.

Tovuti ya L’Equipe inaeleza licha ya mazungumzo ya wawakilishi wa fundi huyu na Al-Hilal bado kuna uwezekano mkubwa akatua Man United ikiwa mashetani hao watafikia makubaliano na mabosi wa PSG.

Wakala wa fundi huyu Rafael Pamenta amefunguka kumekuwa na ofa nyingi, ikiwa pamoja na zile za timu kadhaa kutoka Italia.

Makala: Jonas Savimbi - Mtoto wa kota za Reli aliyegeukia uasi
Liverpool inajiamini kwa Gravenberch