Hatimaye Mlinda Lango wa zamani wa Ligi Kuu England, Ben Foster ametangaza kustaafu soka.

Mchezaji huyo mwenye miaka 40, alishatangaza kustaafu Septemba mwaka jana baada ya kuondoka Watford kama mchezaji huru.

Hata hivyo, aliamua kurudi uwanjani Machi mwaka huu na kusaini kuchezea Wrexham kwa mkataba wa muda mfupi.

Foster alisaidia miamba hiyo maarufu kama Red Dragons kupanda daraja baada ya miaka 15.

Baada ya hapo alisaini mkataba wa mwaka mmoja baada ya kutoka katika sherehe za kupanda daraja zillzofanylka mjini Las Vegas.

Lakini baada ya michezo miwili ya msimu wa 2023/24 ya League Two, kipa huyo ameamua kutangaza kustaafu tena.

Robertinho afichua siri za Maproo Simba SC
JKT Queens yatamba Kampala-Uganda