Rais wa Shirikisho la Soka nchini Hispania ‘RFEF’ amejibu mapigo juu ya kushutumiwa kumbusu mchezaji wa timu ya taifa ya wanawake iliyotwaa Kombe la Dunia kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya England juzi Jumapili (Agosti 20).

Wakati Jenni Hermoso akipokea Medali, bosi huyo wa FA, Luis Rubiales mwenye umri wa miaka 45, aliyekuwa karibu na Rais wa FIFA, Gianni Infantino alikuwa akiwaponge- za wachezaji.

Rublales alianza kushutumiwa baada ya kuonekana akimbusu Hermosa mdomoni, kitu ambacho kilimfanya kupewa majina mengi mabaya.

Alipoulizwa mchezajl mwenyewe, Hermoso alikiri kutofurahla jambo hilo na Rubiales.

Hata hivyo, bosi huyo aliwashutumu wote waliomkosoa akiwaita wapumbavu, huku akisisitiza kuwa tukio hilo lilikuwa la furaha.

Mikopo kausha damu yamuibua RC Manyara
Othman ataja fursa ukuzaji wa Uchumi, maendeleo