Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima amesema uanzishaji wa mfumo wa ramani ya utambuzi wa Mashirika yasiyo ya kiserikali utasaidia kutatua changamoto za upatikanaji wa taarifa muhimu kwa Umma, kuhusu Mashirika hayo.

Dkt. Gwajima ameyasema hayo jijini Dodoma na kudai kuwa mfumo huo utawezesha wananchi na wadau kufuatilia na kujua namna Mashirika hayo yanavyofanya kazi ya utekelezaji wa miradi mbalimbali katika maeneo yao na jinsi wanavyoweza kupata fursa ya kunufainika nayo.

Amesema “nimeunda kikosi kazi maalum kwa ajili ya kuratibu na kuzileta NGOs pamoja kwenye majadiliano ya jinsi gani kuimarisha uelewa wa jamii kwenye utekelezaji wa shughuli za maendeleo ambapo pia Wahe. Wabunge watapata fursa ya kujenga uelewa kwa upana zaidi.”

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima.

Awali akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Idara ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali, Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. John Jingu alisema kwa mwaka huu Wizara imesajili na kuratibu Mashirika 9687.

Alisema, kati ya hayo Mashirika ya kimataifa ni 578, Kitaifa 8001, Kimkoa 464 na Kiwilaya 647 na yanatekeleza afua mbalimbali katika maeneo tofauti nchini, huku akiongeza kuwa Wizara kupitia Ofisi ya Msajili wa NGOs inafanya mafunzo mbalimbali, ili kuwapa elimu na kufuata taratibu na Sheria zilizopo.

Tumejionea tukio la kihistoria, tutalitangaza - Mchengerwa
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Agosti 23, 2023