Baada ya kuota mbaya mechi ya Simba SC na Coastal Union ambayo iliombwa ichezwe keshokutwa ljumaa (Agosti 25), mastaa wa timu hiyo wamepewa mapumziko ya siku nne kuanzia leo Jumatano (Agosti 23) na watarejea kambini Jumapili (Agosti 27).

Simba SC iliandika barua Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) ili mechi hiyo ya raundi ya tatu ya Ligi Kuu Bara ambayo haijapangiwa tarehe ili ichezwe kupunguza viporo lakini baadaye bodi hiyo haikujibu maombi hayo.

Awali kupitia Afisa Habari wa Simba SC, Ahmed Ally alisema wamekubaliwa mechi hiyo ichezwe lakini baadae makubaliano hayo yaliota mbawa.

Simba SC baada ya mechi yao na Dodoma Jiji iliyochezwa Uwanja wa Uhuru, Jumapili na kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 juzi Jumatatu timu hiyo iliingia kambini kujiandaa na mechi yao na Wagosi wa Kaya ambapo jana baada ya bodi kusisitiza ratiba kutokuwa na mabadiliko yoyote kocha Robertinho aliamua kuwapa mapumziko wachezaji wao.

Afisa Habari wa TPLB, Karim Boimanda ambaye amekiri kupokea barua ya maombi ya Simba SC, lakini kilichopelekea kutofanya mabadiliko ya ratiba yao ya ligi ni kutokana na muingiliano wa mechi ya timu ya Taifa Stars inayotarajia kuchezwa kuanzia Septemba 4 hadi l2 mwaka huu ambapo Stars watacheza dhidi ya Algeria.

“Ni kweli waliandika barua ya kuomba mechi ichezwe ljumaa lakini sababu ya mechi hiyo kutopangiwa tarehe kutochezwa hiyo ljumaa waliyoomba Simba SC ni kutokana na ratiba ya Taifa Stars ambao wana mechi ya kufuzu.

“Kikawaida kocha wa timu ya taifa anatakiwa aingize timu kambini wiki kama mbili kabla ya mechi.

“Sasa wiki hizi zipo ndani ya ratiba ya Taifa Stars, kikanuni pia ni kwamba timu ikitoa wachezaji watatu kwenda timu ya taifa basi mechi zake zinasogezwa na Simba SC huenda wakatoa wachezaji hao.

“Hivyo hapa ratiba inatubeba wote ili tuwe salama, bodi na timu, maana kama tungeipangia tarehe hiyo mechi na ikatokea Simba SC imetoa wachezaji zaidi ya watatu wana uwezo wa kugomea mechi kuwa hawatacheza wachezaji wao wapo timu ya taifa,” amesema na kuongeza;

“Hivyo hadi muda huu ratiba ipo pale pale, Simba SC wasubiri hadi bodi itakapopanga tarehe ya mechi hiyo, ukiangalia pia Coastal Union wamewapa mapumziko wachezaji wao.”

Spurs yamtega Romelu Lukaku
Mashabiki Man Utd wamkomalia Pellistri