Tottenham Hotspur imeripotiwa kumtazama Mshambuliaji wa Chelsea, Romelu Lukaku kama usajili muhimu wa kufanya kwenye dirisha hili kabla ya kufungwa, lakini mshambuliaji huyo mwenyewe hana mpango wa kujiunga na miamba hiyo ya Ligi Kuu England.

Lukaku, mwenye umri wa miaka 30, alitumikia msimu wa 2022-23 kwa mkopo huko Inter Milan akitokea Stamford Bridge, akiwa kwenye sehemu ya kikosi cha miamba hiyo ya Italia waliofanya vyema kwenye Serie A.

Lukaku aliisaidia miamba hiyo ya Serie A kufika fainali ya Lukaku Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu uliopita, ambapo Manchester City ilibeba taji hilo katika fainali iliyofanyika Istanbul, Uturuki.

Mabao 10 na asisti sita katika mechi 25 za ligi ulikuwa mchango wa Mshambuliaji huyo wa Kibelgiji kwenye kikosi hicho cha Inter Milan, lakini majaliwa yake ya kukipiga Chelsea yapo kwenye mashaka makubwa, jambo linalowafanya Spurs kuhitaji huduma yake akachezee kwao.

Lukaku ambaye amecheza Anderlech, Everton, Man United, Inter Milan, Chelsea na West Bromwich, hayupo kwenye mipango ya kocha Mauricio Pochettino huko Chelsea, licha ya miamba hiyo ya Stamford Bridge kutokuwa na Namba 9 wa maana kikosini.

Lukaku hakucheza mechi yoyote ya Chelsea kwenye Pre-Season na hata kwenye mechi ilizocheza kwenye Ligi Kuu England msimu huu na klabu hiyo inafanya mchakato wa kuachana naye kabla ya dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi kufungwa.

Mwakinyo kuzichapa na Mkenya
TPLB yafunguka ombi la Simba SC