Kiongozi wa kundi la mamluki wa Urusi – Wagner, Yevgeny Prigozhin anadaiwa kuwa ni miongoni mwa abiria waliokuwa kwenye ndege binafsi ilioanguka hapo jana jioni (Agosti 23, 2023), katika mji wa Tver uliopo zaidi ya kilomita 100 kaskazini mwa jiji la Moscow, ingawa hakuna chombo  kilichothibitisha ikiwa ni kweli alikua ndani ya ndege hiyo.

Shirika la Habari la Urusi -TASS, linasema miili ya watu wanane imepatikana kwenye eneo la ajali, huku mamlaka ya usafiri wa ndege ys Urusi ikisema kulikua na majina ya watu 10 kwenye orodha ya abiria wa ndege hiyo iliyokua inatoka Moscow kuelekea St. Petersburg, na inasemekana kuwa ndege hiyo ilibeba marubani watatu na abiria saba. 

Kiongozi wa kundi la mamluki wa Urusi – Wagner, Yevgeny Prigozhin.

Prigozhin, ana kundi lake binafsi la wanajeshi la Wagner lililopigana pamoja na jeshi la kawaida la Russia huko Ukraine, na lilifanya uasi wa muda mfupi dhidi ya uongozi wa kijeshi wa Russia mwishoni mwa mwezi Juni huku Ikulu ya Kremlin ikisema Prigozhin atapelekwa kuishi uhamishoni Belarus, na wapiganaji wake wangestaafu, kumfuata alipo au wajiunge na jeshi la Urusi.

Video za mtandao wa kijami zilizotangazwa na Wagner zilionesha picha ambazo hazikuweza kuthibitisha za mabaki ya ndege ikiungua zikidaiwa kuwa ni za ajali hiyo na ikumbukwe kuwa pia hivi karibuni, kulisambaa picha zinazonesha Prigozhin akiwa Afrika.

Mradi wa maji Butimba wafikia asilimia 94
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Agosti 24, 2023