Uongozi wa Klabu ya KMC FC umewaomba radhi mashabiki wa klabu hiyo kufuatia kichapo kizito walichokipokea katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2023/24 jana Jumatano (Agosti 23), dhidi ya Mabingwa watetezi Young Africans.

KMC iliyokuwa ikicheza mchezo wake wa pili mzimu huu, ilikuwa ugenini katika Uwanja wa Azam Complex, huku Young Africans ikicheza mchezo wake wa kwanza msimu huu.

Uongozi wa KMC FC umewataka radhi Mashabiki wa klabu hiyo kupita taarifa rasmi iliyochapishwa katika vyanzo vya habari za klabu hiyo ambayo ilikubali kichapo cha 5-0.

Taarifa hiyo imeandikwa: Menejimenti ya timu, benchi la ufundi na wachezaji tunatoa pole kwa mashabiki wetu wote, tunatambua hayakuwa matokeo tuliyotarajia.

Mchezo umekwisha na sasa benchi la ufundi litafanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza na kujiweka imara zaidi kuelekea mchezo uliopo mbele yetu dhidi ya JKT Tanzania (15/09/2023) Tunapoteza pamoja, Tunashinda Pamoja.

Sisi ni Kino boys.

Imetolewa na

Idara ya habari na mawasiliano   

Siah Malle anavyoibua vipaji Wanawake wenye ndoto kubwa
Mradi utunzaji Rasilimali Bahari wanufaisha Vijiji Tanga