Mamia ya Wakazi wa Mji wa Handeni wamejitokeza kushuhudia shehena ya mabomba kwa ajili ya Mradi mkubwa wa maji wa kimkakati Handeni (HMT), wa Miji28 ambayo yamewasili Wilayani humo.

Mabomba hayo, yamepokelewa mapema hii leo Agosti 24, 2023, na kufufua matumaini ya wananchi wa Wilayani humo ya kuondokana na changamoto ya upatikanaji wa maji safi na salama.

Mradi huo ni ahadi ya muda mrefu hivyo limekua ni jambo la faraja sana kwa wana Handeni wakishuhudia Utekelezaji wake chini ya Uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan.

Utekelezaji wa Mradi huu tayari umeanza na kuwasili kwa mabomba haya ni dalili kwamba utamalizika kwa haraka na wakati, ili kukidhi matarajio ya wananchi ambao wana changamoto kubwa ya Maji.

Serikali yatangaza nafasi 6800 za Wanagenzi
Robertinho kufyeka watatu Simba SC