Beki wa pembeni wa Manchester City, Joao Cancelo anatarajiwa kuwasili jijini Barcelona kukamilisha uhamisho wa dili la staa huyo katika dirisha hili.

Inadaiwa wakala huyo ambaye ni Jorge Mendes atakutana na mabosi wa Barcelona kwa lengo la kujadili dili la Ansu Fati anayedaiwa kuomba kuondoka lakini pia atajadili dili la Cancelo anayehitajika na wababe hao.

Cancelo mwenye umri wa miaka 29, anataka kuondoka Man City kwa sababu hapati nafasi ya kutosha kwenye kikosi cha kwanza cha Man City, msimu huu akiwa hajacheza hata mechi moja.

Msimu uliopita alicheza kwa mkopo Bayern Munich ambayo haikuonekana kushawishika kutaka kumsajili mazima licha ya kucheza mechi 21 za michuano yote.

Azam FC: Kulipa kisasi ni haki
Rasmus Hojlund kuivaa Nottingham Forest