Klabu ya Chelsea bado inamtaka mshambuliaji wa Arsenal, Folarin Balogun, baada ya mazungumzo ya awali na Washika Bunduki hao, lakini kwa sasa hawako tayari kufikia bei inayotakiwa ya Pauni Milioni 50.

Chelsea wanatafuta mshambuliaji mpya wa kumpunguzia mzigo Nicolas Jackson na wanamlenga zaidi Balogun, ambaye alifunga mabao 21 katika kipindi cha mkopo akiwa na Stade Reimns ya Ufaransa msimu uliopita.

Baada ya kuwasiliana na wawakilishi wa mchezaji huyo wa Arsenal, Chelsea bado wana nia ya kutaka kumnunua mshambuliaji huyo raia wa Marekani ingawa, imefahamika kuwa The Blues hawako tayari kulipa kiasi cha Pauni Milioni 50 kinachotakiwa.

Hivi karibuni ofa ya Monaco ya pauni milioni 30 kwa Balogun ilikataliwa, huku nia ya mapema ya Inter Milan kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 ilitoweka haraka pale bei ya Pauni Milioni 50 ilipowekwa.

Chelsea inatarajia kumsajili mshambuliaji mpya kabla ya dirisha la usajili kumalizika na pia wanataka mshambuliaji mpya mahiri ambaye anaweza kusaidia kuziba pengo la Christopher Nkunku, ambaye alicheza kama namba 10 na winga katika mechi za kujiandaa na msimu kabla ya kuumia goti.

Uhamisho wa nyota wa Crystal Palace, Michael Olise ulikuwa karibu kukamilika kabla ya Mfaransa huyo kutia saini mkataba mpya, na kuifanya Chelsea kulazimika kufikiria chaguzi mbadala.

Nia inasalia kwa Mohammed Kudus wa Ajax, ambaye West Ham United imeshindwa katika ofa zake mbili.

Ajax ya Uholanzi inasemekana kushikilia dau la Euro Milioni 50 na wameonya hadharani wanaomtaka Kudus wataongeza bei wanayotaka wakati tarehe ya mwisho ya kuhama inakaribia.

Chelsea pia inahusishwa na mpango wa kuwawinda wachezaji wawili wa Lyon, Rayan Cherki na Bradley Barcola

Msuva kutambulishwa rasmi JS Kabyile
Wapongezwa kwa kutumia vyema nafasi za Ubunge