Mshambuliaji Simon Msuva muda wowote anatarajiwa kutangaza na Uongozi wa JS Kabyile ya nchini Algeria, baada ya kumaliza taratibu za usajili.

Msuva hapo awali alikuwa akihusishwa na timu kubwa za hapa nchini Simba SC na Young Africans kwenye usajili huu mkubwa lakini ameamua kwenda kuendelea kucheza nje.

Taarifa kutoka Algeria zinaeleza kuwa, jana Alhamis (Agosti 24) Msuva alikamilisha vipimo vya afya na alikuwa anatarajia kusaini mkataba wa miaka miwili na JS Kabyile ambayo ni moja ya klabu kubwa barani Afrika.

Msuva anajiunga na JS Kabyile akiwa mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake na timu ya AI Quadsiah iliyokuwa inashiriki Ligi Daraja la Pili nchini Saudi Arabia.

Fluminense yaiwekea ngumu Liverpool
Usajili wa Folarin Balogun waibananisha Chelsea