Rais wa Urusi, Vladimir Putin amevunja ukimya kwa kutoa salam za rambirambi na kusema amehuzunishwa na kifo cha Kiongozi wa Kundi mamluki la wapiganaji la Wagner, Yevgeny Prigozhin.

Putin, metuma salamu zake za rambirambi kwa familia za waliopoteza maisha, na kumuelezea mwanzilishi huyo wa Wagner Group, Yevgeny Prigozhin kama mfanyabiashara mwenye talanta.

Katika hotuba yake kwa njia ya Luninga, Putin, amesema wachunguzi watafuatilia nini kilichotokea, lakini suala hilo litachukua muda huku akidai kuwa licha ya Prigozhin kufanya makosa lakini amehuzunishwa na kifo chake.

Yevgeny Prigozhin alikuwa ni miongoni mwa abiria waliokuwa kwenye ndege iliyoanguka Agosti 23, 2023 katika mji wa Tver, uliopo zaidi ya kilomita 100 kaskazini mwa jiji la Moscow, huku Shirika la Habari la Urusi -TASS, likisema miili ya watu nane ilipatikana eneo la ajali na mamlaka ya usafiri wa ndege ya Urusi ikidai kulikua na watu 10.

Hussein Kazi aahidi kazi Simba SC
Laporte amfuara Ronaldo Al-Nassr