Mshambuliaji wa Arsenal, Gabriel Jesus ameonekana akifanya mazoezi na wachezaji wa kikosi cha kwanza na inasemekena atakuwa fiti kuelekea mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Manchester United baada ya mechi za kimataifa.

Mshambuliaji huyo amekosa mechi za ufunguzi za Arsenal baada ya kupata jeraha la goti katika michezo ya kujiandaa na msimu mpya.

Alifanyiwa upasuaji mdogo kuondoa tatizo katika eneo la goti, lakini kocha Mikel Arteta hakuweka wazi tarehe maalumu ya kurudi uwanjani, ila kuna uwezekano ajarejea baada ya mechi za kimataifa.

Kutokana na kinachoendelea, Eddie Nketiah ataendelea kucheza katika safu ya ushambuliaji kwani alionyesha kiwango kizuri katika michezo miwili ya mwanzo ya Ligi Kuu England kwa kufunga na kutoa asisti.

Na sasa mashabiki wa Arsenal wamepata ahueni baada ya Mshambuliaji huyo kuanza mazoezi ya kujiweka fiti kabla ya kurejea kukiwasha.

Pia, mashabiki wa Arsenal waliandika ujumbe mbalimbali kupitia mitandao ya jamii ya X na Instagram kufuatia kurejea kwa mshambuliaji wao.

Shabiki mmoja aliandika “Miujiza”. Baada ya kumuona Jesus kupitia video akifanya mazoezi.

Mwingine aliandika: “Ni mchezaji hatari tutabeba ligi”, Shabiki mwingine wa tatu akadai: “Mtaalamu wa Emirates amerudi rasmi.”

Kitasa cha Zambia chatua Namungo FC
Konkoni amfurahisha Kocha Young Africans