Kinda wa FC Barcelona, Pedro González anaweza kuwa nje ya uwanja kwa mwezi mmoja zaidi, baada ya kuumia nyama za paja wakati anafanya mazoezi.
Kiungo huyo alikuwa tegemeo la ushindi wa FC Barcelona dhidi ya Cadiz wikendi iliyopita akifunga bao katika mechi iliyokuwa na upinzani mkali.
Hata hivyo, Pedri kwa mara nyingine alipata jeraha ambalo linaweza kumfanya kuwa nje ya uwanja muda mrefu.
Jeraha la Pedri ni pigo kwa FC Barcelona ambayo imeanza kutetea ubingwa kwa suluhu na Getafe, katika mchezo wa kwanza na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Cadiz katika mechi ya pili ya LaLiga.
Xavi Hernandez bado ana machaguo mengi ya wachezaji kwani lkay Gundogan, Gavi, Frenkie de Jong na Oriol Romeu anaweza kuwatumia kuelekea FC Barcelona ilitoa taarifa ya kuthibitisha jeraha hilo: “Mchezaji wa kikosi cha kwanza cha FC Barcelona, Pedri amepata jeraha la mguu wa kulia. Atakosekana kwa muda na atarejea endapo atapona.”
Inasemekana Pedri hatakosa michezo ya La Liga dhidi ya Villarreal na Osasuna, lakini pia hatakuwepo katisa kikosi cha timu ya taifa ya Hispania kwa ajili ya kujiandaa na mechi mbili za kufuzu Euro 2024 dhidi ya Georgia na Cyprus mwezi ujao.