Waziri wa mawasiliano nchini Gabon, Rodrigue Mboumba Bissawou ametangaza uzimaji wa inteneti, marufuku ya kutoka nje usiku wakati zoezi la upigaji kura likimalizika nchini Jumamosi.

Bissawou ametangaza hatua hiyo kupitia Televisheni ya Taifa akieleza kwamba hali hiyo itasaidia kukabiliana na kusambaa kwa wito wa ghasia na taarifa za uongo.

Hatua hiyo inafuata malalamiko ya upinzani kuhusu hitilafu zilizoshuhudiwa katika uchaguzi Jumamosi huku mpinzani mkuu katika uchaguzi huo wa urais, Albert Ondo Ossa anadai kulaani alichokitaja kuwa “uongo uliopangwa.”

Hata hivyo, Msemaji wa muungano rasmi wa upinzani, Alternance 2023, amezitaja hatua hizo za serikali kuimarisha usalama kama hatua zilizovuka mpaka na kuongeza kwamba mamlaka hazitaki kuona maendeleo ya demokrasia nchi humo.

Raia wamepiga kura nchini kumchagua rais, wabunge na madiwani huku vituo kadhaa vya kupiga kura vilichelewa kufungiliwa.

Wananchi waunga mkono Jeshi kumtimua Balozi
Serikali yapongezwa uwepo mazingira bora uwekezaji