Kocha Mkuu wa Young Africans, Miguel Gamondi ameweka wazi kuwa licha ya viwango vya mastaa wake ikiwa ni Maxi Mpia, Pacome Zouzoua bado anaamini kuwa hawajaonyesha kwa asilimia 100 kutokana na uwezo walionao.

Pacome na Maxi ni maingizo mapya ndani ya Young Africans tayari wameshaanza kuonyesha makeke yao kikosini hapo baada ya kufanya vyema katika michezo miwili ya mwisho waliyocheza.

Pacome katika michezo iliyopita dhidi ya KMC FC na  ASAS Djibout alifanikiwa kufunga mabao 2 sawa na Maxí ambaye alitoa pasi mbili za mabao katika michezo hiyo.

Kocha Gamondi amesema kuwa licha ya watu kuona kuwa mastaa wake wapya wanafanya vyema lakini kwa upande wake anaamini bado mastaa hao hawajafanikiwa kucheza kwa ubora wao kwa asilimia zote.

“Naamini bado hawachanganya vyema, Pacome ukimtazama utaona tunajaribu kumpa nafasi, kwa kuwa bado hajawa fiti asilimia zote, kwa upande wa Maxi yeye pia hakucheza kwa muda kidogo japo huwezi kuliona hilo.

“Hivyo naamini tunavyozidi kucheza wachezaji wanazidi kuchanganya taratibu na mwisho wa siku tutakuwa vyema na watakaa sawa zaidi ya sasa,” amesema kocha huyo.

Waziri asimamishwa kazi kwa usaliti
Robertinho: Tunaifahamu Power Dynamos