Waziri Katiba na Sheria, Dkt. Damas Ndumbaro amesema zaidi asilimia 50 ya Wananchi hawajui katiba ya nchi na kueleza kuwa wanalo jukumu la kuendelea kutoa elimu juu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Dkt. Ndumbaro ameyasema hayo katika kikao kilichowakutanisha Mawaziri wa Sheria na Wanasheria Wastaafu na waliopo madarakani na Viongozi mbalimbali kwenye majadiliano ya Katiba mpya na mkakati wa elimu ya Katiba ya Tanzania ya mwaka 1977 kwa umma (MTEKU 2023/2026).

Kikao hicho, pia kimetolea ufafanuzi kwa baadhi ya watu ambao wanaodai katiba mpya kwani wameshaunda kamati ambayo itafanya mchakato wa katiba mpya.

Naye, Waziri mstaafu, Mary Nagu, amesema wananchi wanapaswa kujua katiba kikamilifu ikiwemo katiba ya mwaka 1977 na kujua kitu gani kimepungua na kipi kimezidi endapo watafanya mabadiliko katika katiba mpya na kama kuna mabadiliko yafanyike na sio kuleta katiba mpya kila wakati.

Kocha Power Dynamos aingia ubaridi
Gari la Maiti latumika kusafirisha Bangi, harufu yawakamatisha