Mkoa wa Singida umefikiwa na harufu ya utalii wa Akiolojia, Utamaduni na Malikale, baada ya
ugunduzi wa maeneo mapya ya masalia ya binadamu wa kale, zana za Mawe na  michoro ya Miamba katika Kijiji cha Siuyu kilichopo Wilaya ya Ikungi.

Akizungumza na watafiti wa Akiolojia kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Katibu Tawala Wilaya ya Ikungi,  Rashid Rashid ameipongeza Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Idara ya Malikale nchini, kwa juhudi inazozichukua katika tafiti zinazoibua maeneo mapya yenye historia adhimu ya Binadamu wa kale eneo la Siuyu Singida.

Amesema, jamii inatakiwa kuhakikisha maeneo hayo ya Malikale yanalindwa kwa maslahi ya wanaikungi na Taifa kwa ujumla, huku akiahidi kuwa Serikali ya Wilaya itaendelea kushirikiana na Wizara ya Maliasili katika uhifadhi na kutangaza vivutio vya Malikale.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Malikale nchini, Dkt. Christowaja Ntandu amesema matokeo chanya ya tatifi zinazofanywa licha tu ya kuongeza kasi ya utalii na uchumi wa nchi pia zinatoa elimu kwa jamii juu ya mabadiliko ya tabia ya nchi na umuhimu wa uhifadhi endelevu na utunzaji wa mazingira.

Awali, Mtafiti wa akiolojia kutoka Chuo Kikuu cha Sapienza nchini Italia, Prof.  Marina  Gallinaro alisema  kutokana na utajiri mkubwa wa maeneo ya Malikale hapa nchini hasa Mkoani Singida,  amevutiwa kuja nchini kuungana na watafiti wa nchini Tanzania kufanya utafiti.

Kitayose yaichimba mkwara Singida FG
Kocha Power Dynamos aingia ubaridi