Beki wa zamani wa Klabu ya Chelsea, Marcos Alonso ametajwa kuwa katika harakati za kurudi tena katika Ligi Kuu ya England msimu huu 2023/24.

Manchester United imeripotiwa kuwa katika mipango ya kumsajili beki huyo wa kushoto wa FC Barcelona kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili.

Mashetani Wekundu wameingila sokoni kutafuta beki ambaye ataziba nafasi ya Luke Shaw, aliyeumia na kuwa nje ya uwanja kwa miezi kadhaa akisumbuliwa na misuli.

Mchezaji aliyekuwa kwa ajilil ya kubadilishana naye, Tyrell Malacla pia atakuwa nje kwa muda mrefu baada ya kushindwa kupona kwa wakati akiumia tangu msimu ulopita.

Mtu wa kwanza anayeangaliwa ni beki wa sasa wa Chelsea, Marc Cucurella, ambaye si chaguo la kwanza la Maurlcio Pochettino, ikiwa ni mwaka mmoja tangu aliposajiliwa.

Robertinho aomba mechi za kirafiki
Simon Msuva aibua shangwe JS Kabylie