Baada ya Kikosi cha Simba SC kurudi kambini na kuanza mazoezi, Kocha Mkuu wa timu hiyo, Oliveira Roberto ‘Robertinho’ amesema siku 30 za mapumziko zinahitaji mechi za kirafiki ili kuweka kikosi chake kwenye ushindani.

Kesho Jumatano (Agosti 30) kutakuwa na mchezo mmoja wa ligi na baada ya hapo ligi itasimama kwa muda kupisha mchezo wa kufuzu kwa Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON), wakati Taifa Stars ikimenyana na Algeria.

Simba SC inaingia kambini na leo Jumanne (Agosti 29) na kuanza mazoezi tayari kwa ajili ya kujiweka sawa na mechi za Ligi Kuu, Ligi ya Mabingwa Afrika na Super League, mashindano ambayo kocha amekiri kuwa anahitaji kikosi kilicho timamu.

“Timu imecheza mechi mbili na kupata mapumziko, nahitaji kuwa na mazoezi mepesi na ya nguvu, lengo ni kuitengeneza timu ya ushindani ndani ya dakika zote 90, haitakuwa rahisi kama tutafanya mazoezi bila mechi za kirafiki.

“Nimeongea na viongozi kuhakikisha wananitafutia timu ambazo zitawapa changamoto wachezaji, lengo ni kujenga utimamu na kuwapa pumzi, kwani tuna mashindanio mengi mbele,” amesema Robertinho.

Kocha huyo raia wa Brazil amesema ratiba ya ligi haijawa rafiki kwao kukiweka kikosi chao katika mfumo mzuri wa kuzoeana baada ya kucheza mechi mbili na kupata mapumziko.

Robertinho amekiri kuanza vizuri lakini anaanza upya kutokana na sifa za wachezaji kutokuwa pamoja ndani ya muda kunavyowafanya kujiweka fiti upya, huku akiweka wazi kuwa wachezaji ni kama watoto wanaohitaji muda wote kuelekezwa.

Virgil van Dijk hatarini kufungiwa England
Man Utd yampigia hesabu Marcos Alonso