Aliyewahi kuwa Kocha Mkuu wa Yanga Princess, Edna Lema ambaye kwa sasa yupo Biashara United ya Mara ameipa nafasi kubwa JKT Queens kutwaa ubingwa wa Klabu Bingwa ya Soka la Wanawake kwa Nchi za Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) na kuitaka iondoe hofu.

JKT Queens imetinga Fainali baada ya kuichapa Buja Queens mabao 3-1 yaliyofungwa na Donisia Minja ambaye katika mechi nne ana mabao manne, Stumai Abdallah mwenye mabao mawili na Winfrida Gerald.

Fainali hiyo hiyo inatarajiwa kupigwa kesho Jumatano (Agosti 30) katika Uwanja wa Njeru nchini Uganda ambapo JKT itakutana na CBE ya Ethiopia iliyofika hapo kwa kuichapa Vihiga Queens mnabao 2-1.

Edna amesema kutokana na ubora wa JKT waliouonye sha katika mechi nne unatosha kuiwezesha kubeba ubingwa ambao watetezi ni Simba Queens waliomaliza nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara ya Wanawake.

Amesema Tanzania imekuwa ikifanva vizuri kitika soka la wanawake hasa kimataifa, hivyo Wanajeshi hao Wa kike wanatakiwa kupunguza presha ya fainali na kuingia kwa tahadhari na kushambulilia zaidi.

“Nimeitazama JKT mechi ilizocheza naiona ikibcba ubingwa kwa asilimia kubwa kwa sababu ina kikosi kizuri na kipindi hiki ni natasi yao kuleta komlbe, kwani CRE wanafahamiaa vizuri kwa kuwa waekutana mara Ivingi muhinu ni upunguza presha, amesema Lema.

JKT ilikata tiketi ya Fainali baada ya kuifunga New Generation bao 1-0 huku ikimaliza kinara wa kundi B kufuatia kushinda mechi zote tatu na kukusanya pointi tisa.

Greenwood aachwa njia panda
Virgil van Dijk hatarini kufungiwa England