Mason Greenwood amebaki njiapanda juu ya hatma ya soka lake baada ya Manchester United kuchukua uamuzi wa kumpiga chini na hakuna timu inayoonesha wazi kuhitaji huduma yake.

Na sasa matumaini ya mshambuliaji huyo yamebaki kwenye klabu moja huko Albania, mahali ambako anaweza kwenda kucheza baada ya kutokuwapo na timu za kutoka Ligi Kuu tano bora za Ulaya kumhitaji.

Greenwood mwenye umri wa miaka 21 na familia yake alikuwa na matarajio makubwa ya kurudi kuichezea Man United baada ya mabosi kuonesha wangempa nafasi nyingine ya kuonyesha ubora.

Lakini, baada ya kelele za raia wengi kupinga uamuzi wa Man United kumrudisha kutokana na kile alichofanya na kuwafanya mabosi wa miamba hiyo ya Old Trafford kutangaza kuachana naye.

Matumaini yake ya kuanza upya maisha kwenye soka yalikumbwa na pigo kubwa baada ya taarifa kutoka Italia, hasa Klabu ya AS Roma inayonolewa na Jose Mourinho iliyokuwa ikiripotiwa kuhitaji saini yake kusitisha mpango huo, huku Klabu za Saudi Pro League zikifunga milango ya kumpokea.

Greenwood alikuwa akikabiliwa na mashtaka ya jaribio la kubaka na unyanyasaji kijinsia yaliyomfanya awe nje ya uwanja muda mrefu kabla ya kufutwa.

Tangu kutokea kwa tukio hilo kumekuwa na kampeni za kutocheza tena kwenye soka a England, lakini jambo hilo limekuwa likimwandama hadi nchi nyingine na sasa matumaini yake yamebaki huko Albania, ambako kuna klabu moja inaweza kumchukua.

Julai mwaka huu, Greenwood alipata mtoto na mwanamke aliyedaiwa kutaka kumbaka.

Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Man United, Richard Arnold, alisema kwenye uchunguzi maalumu uliofanywa na klabu kwa miezi mitano uligundua hakufanya kosa lolote, lakini mwenyewe ametaka kuondoka ili kwenda kuendelea na soka lake.

Azizi Ki aibua gumzo Soka la Bongo
Kocha Yanga aipa ubingwa JKT