Kiungo Mshambuliaji wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans, Max Nzengeli Mpia amesema kwa kikosi alichokikuta klabuni hapo, ana uhakika kitafika mbali kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika, huku mwenyewe akijiandaa kuipa mafanikio klabu hiyo ili kurudia kilichofanywa msimu uliopita.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, raia huyo wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo pia amefichua siri ya kupenda kuchomekea jezi, akisema babu yake ambaye alikuwa mtanashati sana alipenda kuchomekea kila anapoonekana.

“Young Africans tuna kikosi kizuri na kocha wetu amekuwa akikibadilisha kwa ajili ya kuwafanya wachezaji wote wacheze ili wawe kwenye Ubora unaofanana,”

“Tuna timu ambayo nina uhakika itafanya vizuri huko mbele ya safari, sisi wachezaji wapya tuna deni ambalo ni kujitahidi na kuhakikisha tunapambana kwa sababu kama msimu uliopita timu ilifika fainali ya Kombe la Shirikisho,”

“Msimu huu sisi tunatakiwa tufanye vema kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, tufike mbali ili turudie kile ambacho wenzetu walikifanya huko nyuma,” amesema mchezaji huyo ambaye pia kuna wakati uwanjani hucheza kama kiungo mshambuliaji.” Amesema Max

Hesabu za CAG hazina mashaka - Mwigulu
Vinicius Jr kuikosa Real Madrid siku 42