Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma, Mathew Kirama ameitaka   Menejimenti ya Tume hiyo kwa kushirikiana na wadau wake kufanya tathmini ya kati ya Mpango Mkakati wa Tume, ili uwaongoze kufanya kazi kwa ufanisi zaidi kuweza kufikia malengo ya Taasisi na Serikali kwa ujumla.

 Kirama ameyasema hayo alipokuwa akifungua kikao kazi cha tathmini ya kupitia Mpango  Mkakati  wa Tume wa mwaka 2021/2022 hadi mwaka 2025/2026, kilichofanyika Septemba 30, 2023 Jijini Dodoma.

Amesema, “tunafanya tathmini kupitia Mpango Mkakati wa mwaka 2021/22  hadi mwaka 2025/2026 na tumefikia muda wa kati. Tunafahamu kumekuwepo na mabadiliko mbalimbali ya Dira, Sera, Sheria, Majukumu ya Taasisi na pia mwelekeo wa Serikali.”

Aidha, Kirqma amefafanua kuwa ni muhimu Tume kujipanga kuwa sehemu ya maono ya nchi na maboresho yanayoendelea kufanyika kuhakikisha  utumishi wa umma unatoa huduma bora zenye kukidhi matarajio ya wananchi na watumishi wa umma.

Akizungumza kuhusu Tume, Kirama amesema, “ni muhimu sana kuangalia tunafanya nini kwa upande wa rasilimali watu, kubadilisha fikra na namna ya kufanya kazi sambamba na kuboresha mifumo yetu ya kimenejimenti na matumizi ya TEHAMA katika kuwahudumia wadau wetu. 

Naye Mkurugenzi wa Kitengo cha Mipango, Ufuatiliaji na  Tathmini kutoka Tume ya Utumishi wa Umma, Abdallah Mvungi amesema  lengo la Kikao kazi hiko ni kufanya tathmini ya utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Tume kwa kipindi cha Kati, ambao ndio dira kuelekea mafanikio na maendeleo endelevu.

Gamondi afunguka ishu ya Konkoni
FA yamfungulia mashtaka Virgil van Dijk