Baada ya kutua katika mji wa Tabarka nchinΓ Tunisia, kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars, jana Ijumaa (Septemba Mosi) hakuna kulala, kilianza mazoezi ya kujiandaa na mchezo wa marudiano wa kufuzu wa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) dhidi ya Algeria.
Stars itakuwa ugenini katika mchezo utakaochezwa Septemba 7, mwaka huu jijini Algers, Algeria huku ikiwa na kumbukumbu ya kukubali kichapo cha mabao 2-0, katika mchezo wa kwanza uliopigwa Uwanja wa Bernjamin Mkapa, Dar es Salaam.
Katika kampeni hizo, Stars imepangwa Kundi F, inashika nafasi ya pili katika msimamo ikiwa na Pointi saba huku Algeria ikiwa tayari imefuzu kwa kujizolea Pointi 15, Uganda ipo nafasi ya tatu ikiwa na Pointi nne wakati Niger ikiburuza mkia nΓ₯ pointi zao mbili.
Katika mchezo huo wa marudiano, Stars inahitaji ushindi wa Pointi tatu au sare kuweza kufuzu katika mashindano hayo.
Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Cliford Ndimbo, amesema kikosi kimeaanza maandalizi ya mchezo huo kuhakikisha kinafanya vizuri.
Kikosi hicho kinachonolewa na kocha Adel Amrouche, kimeanza maandalizi kikiwa na wachezaji 25 huku kipa Beno Kakolanya, akiungana na wenzake jana Ijumaa (Septemba Mosi) jioni baada ya kumaliza mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya timu yake ya Singida Fountain Gate dhidi ya Kitayosce, uliochezwa juzi Alhamis (Agosti 31).
Ndimbo amesema wachezaji wanaocheza nje ya Tanzania wataungana na wenzao kuanzia kesho Jumapili (Septemba 03).
Stars inaundwa na Beno Kakolanya (Singida BS), Metacha Mnata (Yanga), Erick Johora (Geita Gold), Ibrahim Hamad, Bakari Mwamnyeto (Yanga), Mzamiru Yasin (Simba), Sospeter Bajama (Azam), Clement Mzize (Yanga), Kibu Deins (Simba), Himid Mao (TalaEA Gaish Misri), Mudathir Yahya (Yanga) na Abdul Seleman (Azam).
Wengine ni Abdulmalik Zakaria (Namungo), John Bocco, Kennedy Juma (Simba), Lameck Lawi(Coastal Union) na Jonas Mkude wa Yanga.
Morice Abraham (FK Sportak Subotic, Seribia), Haji Mnoga (Aldershot united, Uingereza), Ben Starkie (Basford United, Uingereza), Saimon Msuva (S Kabylie, Algeria), Novatus Dismas (Zulte Waregem, Ubelgj), Mbwana Sarnatta(Paok FC, Ugiriki) na Abdi Banda (Richard Bay F.C, Afrika Kusini).
Pia Kocha Amrouche amemuongeza kikosini beki wa Young Africans, Nickson Kibabage ambaye ameondoka jana Ijumaa (Septemba 01) kwenda kambini nchini Tunisia.