Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Pius Lutumo amefunga mafunzo ya kuwajengea uwezo Wakaguzi wa Polisi toka Wilaya zote na Vikosi vyake vilivyopo Kibaha Mkoani Pwani.

Akifunga mafunzo hayo ya awamu ya pili, Kamanda Lutumo amewataka wakaguzi hao kuwa na utii na kwenda kufanya kazi kulingana na viapo vyao.

Mafunzo hayo yaliyofanyika kwa miezi miwili, yamefungwa katika viwanja vya Polisi Mkoa wa Pwani.

Aidha, aefafanua kuwa hategemei kuona Mkaguzi aliyehitimu mafunzo hayo kufanya kazi kinyume na kiapo chake kwenye kuwahudumia wananchi.

Ukatili: Wanawake, Watoto wahanga wakuu
Kihongole awataka Wanafunzi kuwa na jitihada binafsi