Kiungo Mshambuliaji ‘WINGA’ mwenye vituko vingi ndani na nje ya uwanja aliyewahi kutamba nchini katika klabu za Simba SC na Young Africans, Bernard Morrison ‘BM’ amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuwatumikia mabingwa wa Moroco, FAR Rabat, huku akitakiwa kukaa ndani ya jingo la klabu lililopo katika kambi ya jeshi.

FAR Rabat inamilikiwa na jeshi ikifundishwa na kocha wa zamani wa Young Africans, Nasreddine Nabi.

Licha ya winga huyo kuonyesha kiwango bora katika mazoezi ya kupima ubora wake hatua ya kumpa mkataba huo, haikuwa rahisi kutokana na rekodi mbovu juu ya nidhamu, lakini baada ya kikao kizito na mabosi wa klabu hiyo hatimaye ljumaa (Septemba Mosi) wakampa mkataba huo kuitumikia timu hiyo.

Morrison ambaye ni raia wa Ghana, katika miezi hiyo 12 hatakiwi kufanya matukio yoyote ya utovu wa nidhamu na ikijitokeza mkataba wake utasitishwa mara moja na kuondoshwa klabuni.

Licha ya mkataba huo mgumu, lakini Morrison katika mazoezi ya majuma mawili aliyoyafanya na FAR Rabat amewashtua kwa kiwango kikubwa, huku baadhi ya mastaa wa timu hiyo wakishinikiza asajiliwe.

Winga huyo alitarajiwa kuanza kucheza mwishoni mwa juma lililopita dhidi ya Raja Athletic ukiwa mchezo mgumu wa kwanza pia kwa hapa nchini mchezaji huyo alivitumia vigogo Simba SC na Young Africans kwa nyakati tofauti na kubeba navyo ubingwa.

Nabi ambaye ameshinda mechi zote tatu za mashindano tangu atue Rabat akitoka kuipa Young Africans mataji matatu kwa mpigo ndani ya misimu miwili iliyopita na kuifikisha timu hiyo fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Mecky Mexime afuta kila kitu Kagera Sugar
Vifo vyazidi kuitikisa Sudan 22 wakiuawa