Baada kupangwa na Al Ahly katika mashindano African Football League, Simba SC imesema ipo tayari kucheza na timu hiyo kwa kuwa inahitaji kuionyesha Afrika ukubwa wake.

Simba SC juzi Jumamosi (Septemba 02) ilipangwa kucheza na Al Ahly katika hatua ya Robo Fainali ya michuano hiyo itakayoanza kufanyika Oktoba 20, mwaka huu.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC Ahmed Ally amesema lengo la timu yao hivi sasa ni kutumia mechi kubwa kuonyesha ukubwa wao.

“Tumefurahi kupangiwa Al Ahly. likuwa ni lazima ucheze na timu kama Al Ahly, Wydad Casablanca Esperance. Na sisi katika kampeni yetu ya kutaka kusimika ukubwa wa klabu yetu ni lazima tucheze na Al Ahly. Uzuri ni kwamba wanaifahamu vyema Tanzania,” amesema

Simba SC itaanza nyumbani katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es salaam ambao ndiyo utakuwa ufunguzi rasmi wa michuano hiyo inayofanyika kwa mara ya kwanza Afrika.

Katika ratiba nyingine, TP Mazembe itavaana na Esperance, Enyimba itacheza na Wydad wakati Petro Atletico itavaana na Mamelodi Sundowns.

Gamondi atoa tahadhari Ligi Kuu
Mashujaa FC yasaka pumzi ziwa Tanganyika