Kocha Mkuu wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Miguel Gamondi amezipa tahadhari timu za Ligi Kuu, baada ya timu yake kuanza vema kwa kushinda mechi mbili mfululizo mabao 5-0 walipocheza dhidi ya KMC na JKT Tanzania.

Young Africans pia ilipata ushindi wa mabao 5-1 walipocheza dhidi ya ASAS FC ya nchini Djibouti katika Ligi ya Mabingwa Afrika.

Akizungumza jijini Dar es salaam, Gamondi amesema kuwa timu pinzani hazitakiwi kujilinda zaidi wanapokutana na badala yake kufunguka kwa kucheza soka kama hawataki kufungwa tano.

Gamondi amesema kuwa timu yake inapata ugumu inapokutana na wapinzani wanaocheza soka la pasi na kushambulia, hiyo inawafanya wapate ugumu wa kushambulia.

Ameongeza kuwa timu ikijilinda sana, inawapa nafasi ya wao kufanya mashambulizi kwa kasi huku wakianza kuwakabia kuanzia golini kwa wapinzani.

“Wapinzani wenyewe ndio wanataka tuwafunge mabao matano ni kutokana na kucheza soka la kujilinda kwa kukaa wengi golini kwao.

“Wao kama hawazitaki tano, basi wasijilinde na badala yake wanapaswa kushambulia kwa kucheza soka la pasi.

“Kwani wakijilinda sisi tunapata nafasi ya kushambulia goli la wapinzani kwa kasi tukiwatumia viungo kupiga pasi za mabao,” amesema Gamondi.

Jude Bellingham amvuruga Carlo Ancelotti
Ahmed Ally: Tunataka kuonyesha ukubwa wetu Afrika