Rais wa zamani wa Inter Milan, Massimo Moratti amemjia juu Romelu Lukaku baada ya kujiunga na AS Roma katika dirisha la usajili la kiangazi.

Mshambulizi huyo anayekipiga AS Roma kwa mkopo kutoka Chelsea alicheza mechi yake ya kwanza dhidi ya AC Milan hata hivyo wakapokea kichapo cha mabao 2-1.

Bosi huyo aliiambia Radio Bruno Firenze: “Hata kama Lukaku kaondoka, nadhani Inter inaweza kuwa hatari msimu huu, kikosi chake kimeimarishwa sana hasa sehemu ya kiungo kwani wamesajili wachezaji wengi wazuri. Niliona mechi ya Inter inacheza mpira mzuri sana, Nafikiri Lukaku atajiona mjinga sana.”

Lukaku aliondoka Chelsea baada ya Mauricio Pochettino kuonyesha wazi kwamba hana mpango na fowadi huyo msimu huu, baada ya kurejea akitokea Inter kwa mkopo.

Ikumbukwe alitemvwa pia katika kikosi kilichokwenda Marekani kwa ajili ya ziara.

Aidha, baada ya kutua AS Roma kiungo wa zamani wa Roma, Gaetano D-Agostino alisema Lukaku ataongeza nguvu katika kikosi hicho msimu huu licha ya kupokea kichapo dhidi ya AC Milan.

AS Roma ilimchukua Lukaku kwa mkopo wa msimu mzima ambapo italipa ada ya Pauni 8 milioni baada ya kukubaliana na Chelsea, ingawa kiungo huyo hana matumaini kama Lukaku ataweza kuisaidia AS Roma katika mbio za kuwania ubingwa wa Serie A msimu huu.

D-Agostino alisemaalisema: “Ujio wake utaongeza nguvu katika kikosi, lakini ubingwa sidhani kwa sababu katika idara nyingine timu bado haijakamilika, safu ya ulinzi bado haina nguvu, Jose Mourinho anaweza kubadilisha mfumo pia kwa sababu aina ya mawinga tulionao hawana ubora wa kucheza 3-5-2 na 2-4-2-1.”

Jamii isaidie kutimiza ndoto za Mtoto wa kike - WOWAP
Vijana walia na uhaba vifaa vya kuchunguza VVU