Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Rais wa Kenya, William Ruto mara baada ya kuwasili katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Kenyatta (KICC) kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi Barani Afrika (Africa Climate Summit 23), Nairobi nchini Kenya.
Rais Samia akiwa na Wakuu wa Nchi na Serikali pamoja na Viongozi wa Taasisi mbalimbali za Kimataifa wakati wa Wimbo wa Umoja wa Afrika (AU) na ule wa Taifa wa Kenya ukiimbwa mara baada ya kuwasili katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Kenyatta (KICC), Nairobi nchini Kenya Septemba 5, 2023 kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi Barani Afrika (Africa Climate Summit 23).
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba akiwa pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Selemani Jafo katika Mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi Barani Afrika (Africa Climate Summit 23) Nairobi nchini Kenya.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Makamu wa Rais wa Kenya, Rigathi Gachagua mara baada ya kuwasili katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Kenyatta (KICC) kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi Barani Afrika (Africa Climate Summit 23) Nairobi nchini Kenya.

Wito: PAPU ianzishe mfumo anuani za makazi – Rais Sami

Gary Neville: Rice ni shujaa mpya Arsenal
KITAIFA: GST ni Moyo Sekta ya Madini - Mavunde