Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Patrobas Katambi amesema Serikali imeweka mfumo wa ufuatiliaji na tathmini ya miradi na programu za vijana ili kupima matokeo ya utekelezaji sambamba na kuleta tija kwa Taifa.

Katambi ameyasema hayo Bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti maalum (CCM), Ng’wasi Damas Kamani ambaye ameihoji serikali inatumia mfumo gani kuhakiki ubora na matokeo chanya ya programu zinazotekelezwa na vijana.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri Katambi amesema Serikali ilitoa mwongozo wa kitaifa wa ufuatiliaji na tathmini wa miradi na programu za maendeleo ambapo Ofisi ya Waziri Mkuu imekuwa ikifanya ufuatliaji wa utekelezaji wa programu kila robo mwaka.

Aidha, ameongeza kuwa Serikali imepanga kufanya tathmini mahususi (Tracer Study) ya mafunzo yanayotolewa kupitia programu za kuwezesha vijana ili kubaini mafanikio yaliyopatikana katika kuwezesha vijana kujiajiri au kuajiriwa.

Mike Dean amaliza utata Penati ya Arsenal
Luhemeja ataka ubunifu wa kazi wenye malengo