Mahakama ya Mkoa wa Vuga, imemhukumu mshtakiwa ambaye ni mkazi wa Hawai Zanzibar, Said Salum (28), kutumikia kifungo cha miaka 15 Chuo cha Mafunzo na kulipa fidia ya shilingi Milioni Moja kwa kosa la Kumuingilia kimwili mgonjwa wa akili.

Akisoma maelezo ya hukumu hiyo, Hakimu wa Mahakama, Nayla Abdulbasit Omeyar amesema amejiridhisha na ushahidi uliotolewa na mashahidi saba, ambao haukuwa na shaka uliomtia mshtakiwa hatiani.

Said alishtakiwa kwa kosa la kumuingilia kimwili mgonjwa wa akili kinyume na kifungu namba 133 cha sheria ya adhabu 6/2004 na kesi hiyo ilifunguliwa Mahakamani tarehe Julai 1, 2019 na kupewa kesi namba 203/2019.

Awali ilidaiwa kuwa, Desemba 2, 2017 majira ya saa 11:00 Jioni huko Hawai Wilaya ya Magharibi “B” Mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar, mshtakiwa alimuingilia mwanamke mwenye ugonjwa wa akili, jambo ambalo ni kosa kisheria.

Uhaba wa Mafuta: Malisa awatoa hofu wakazi wa Mbeya
Mgomo kupinga gharama za maisha waanza rasmi